Tanzania

  • mzalendo.net
  • 3 days ago

Na.Abdi Suleiman -Pemba. HATIMAE wajumbe kamati Tendaji ya chama cha soka Zanzibar ZFA Taifa, wamezikataa barua za kujiuzulu kwa Viongozi wa juu wa Chama hicho Zanzibar. Wajumbe wa kamati hiyo waliokutana leo katika ofisi ya ZFA Pemba zilizomo uwanja wa michezo Gombani, huku kikao hicho kikiongozwa na Mwenyekiti wake Sharif Juma Saidi. Akizungumza na waandishi wa habari za Michezo Pemba, mwenyekiti huyo alisema wajumbe wamezikataa barua za viongozi hao wa juu, kwa lengo la kuepuka kadhia ambayo inayoweza kuipata hapo mbele, kutokana na timu za Zanzibar zinatarajiwa kushiriki mashindano mbali mbali ya kimataifa. Alisema awali kabla ya kuanza kikao hicho, walianza kwa kupitia vifungu mbali mbali vya katiba ya ZFA ya 2010, ikiwemo kupata idadi ya wajumbe wa Upande wa Pemba. Alisema Pemba inawajumbe 14 na waliohudhuria katika kikao hicho ni wajumbe 13, huku wakitumia kifungu cha 12 katika katiba hiyo ili kupata maamuzi na kikao vya ZFA, pamoja na kusema kikao hicho kimepata Baraka kutoka kifungu cha 12:2(ii) na kuwa halali. “Kilichotuleta hapa ni kupitia barua ya Makamu wa Rais wa ZFA Pemba Ali Mohamed Ali, aliyowasiliza ZFA juu ya kujuuzulu kwake Juni 13 mwaka huu”alisema. Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuipitia barua hiyo kwa mujibu wakatiba ya ZFA ya 2010, suara ya 12 kifungu cha 92 kimesema bila ya kujali sababu yoyote, mjumbe yoyote anayohaki ya kujiuzulu katika wadhifa alionao, 92:1 kimesema mjumbe hatajiuzulu mpaka apelike kwa tendaji katika ngazi inayohusika, ndipo kifungu cha 92:2 ndicho kilichowapa nafasi ya kusikiliza ombi la mjumbe. “Sisi hapa hatukaja kujadili bali tumekuja kukubali ombi lake au kukataa ombi lake la kujiuzulu wadhifa wake tu”alisema. Aidha alisema baada ya kufikia muwafaka wajumbe waliweza kutumia kifungu cha 36 katika katiba ya 2010 ya ZFA juu ya upigaji wa kura, ili kufikia maamuzi ambapo maamuzi yanaweza kufikiwa kwa njia ya upigaji wa kura, (i) upigaji wa kura utakuwa wa siri kwa kamati tendaji (ii) maamuzi yaweze kuafikiwa na wajumbe. Alisema upigaji wa kura hizo wajumbe 13 waliohudhuria kikao hicho, kura mbili ziliharibuka na kura Tano ziliweza kukubali kujiuzulu kwa makamu huyo wa Rais wa ZFA, huku kura sita ziliweza kumkatalia maamuzi yake ya kujuuzulu wadhifa huo na wajumbe kumtaka katibu wa ZFA Taifa, kumuandikia barua ya kurudi tena katika nafasi yake ya uongozi. “Kutokana na maamuzi hayo ya wajumbe ya upigaji wa kura, kikao hicho hakikuridhia kujiuzulu kwa makamo huyo” huku wakimtaka katibu Mkuu kumuandikia barua ikizingatiwa mbele kuna hatua ya nane bora ya ligi kuu ya zanizbar. Wakati huo huo alisema Kamati hiyo ilikaa kikao Juni 12 ambapo wajumbe walikuwa 10 na kora iliweza kutimia kwa kupitia barua mbili, ikiwemo ya kujiuzulu kwa Rais wa ZAF Ravia Idarous Faina na Mkurugenzi wa Ufundi Abdullghan Mssoma ambayo ilikwenda kwa Rais. Alisema kura 10 ziliweza kumkatalia kujiuzulu kwa Ravia na kumtaka katibu mkuu kumuandikia barua ya kurudi madarakani, huku Mzee Zam Ali akiridhiwa kujiuzulu kwake kutokana na sababu mbali mbali alizozieleza katika barua yake. Zanzinews The post Wajumbe wa Kamati Tendaji ya ZFA Wajiuzuli Uongozi. appeared first on Mzalendo.net.

  • mzalendo.net
  • 5 days ago

By Burhani Yakub – Mwananchi Friday, June 15, 2018 Waislamu wa mji wa Tanga jana Ijumaa, Juni 15 waliungana na wenzao duniani katika sala ya Eid El Fitr na kuonywa kutokubali kutamka maneno yanayodai kuwa uongozi wa Rais John Magufuli umesababisha hali ngumu ya maisha. Walielezwa kwamba maeneo hayo hayapaswi kuzungumzwa na Waislamu kwa sababu yanapingana na maelekezo ya Mwenyezi Mungu, na kwamba waislam wanapoona maisha ni magumu wanatakiwa kujitafakari juu ya matendo yao. Kauli hiyo ilitolewa Ijumaa, Juni 15 na Sheikh Salim Bafadhili wakati akitoa hotuba ya sala ya Eid el Fitr iliyosalishwa na Imam Amin Said (Ammy) katika uwanja wa Tangamano, mjini Tanga. “Msizitukane zama hakika zama ni Allah mwenyewe,” alisema Sheikh Bafadhil wakati akinukuu maneno kutoka katika kitabu kitakatifu cha Qur’an. Aliwataka waislamu wasilalamikie hali ngumu badala yake wajikite katika kufanya ibada na kuepuka maovu ili Mwenyezi Mungu awape wepesi katika upatikanaji wa riziki. Sheikh huyo aliwataka wasilamu kusoma vyema dini yao ndipo watakapobaini kwamba hata walioishi zama za nyuma kuna wakati walikumbana na maisha magumu baada ya kukengeuka maandiko ya Mwenyezi Mungu, lakini waliporejea kwenye ibada ya kweli neema ilirejea. Kuhusu Sikukuu ya Eid, Sheikh Bafadhili aliwahimiza wanawake kuimarisha mema waliyokuwa wakiyafanya wakati wa mwezi wa Ramadhani ikiwamo kuvaa mavazi ya kuwasitiri ili amani na utulivu uliokuwepo uendelee. Katika msikiti mkuu wa Ijumaa mjini Tanga, Sheikh wa Bakwata Mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu aliwaeleza wasilamu kwamba Mwenyezi Mungu waliyekuwa wakimnyenyekea katika mwezi wa Ramadhani yupo miezi yote. Naye, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimuwakilisha Rais John Magufuli kwenye Baraza la Eid el Fitr lililofanyika katika viwanja vya Mnazimmoja mjini Dar es Salaam. Akizungumza kwa niaba ya Rais Magufuli, Majaliwa amewaasa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kutenda mema baada ya kuwa wamejisahihisha na kutubu makosa yao ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Waziri Mkuu alisema viongozi wanaendelea kuwasihi Waislamu wote na Watanzania kwa ujumla kuonyesha upendo, umoja na kuvumiliana hasa baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. “Huruma, ukarimu na ucha Mungu ulionyeshwa katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani, uendelee na uwe sehemu ya maisha ya kila siku na kamwe isiwe umeisha baada ya mfungo wa Ramadhani,” alisema Majaliwa. Waziri Mkuu aliongeza kuwa upendo, umoja, utulivu, mshikamano na subra ulioonyeshwa kipindi chote cha mfungo wa Ramadhani ni vyema vikaendelezwa kwa sababu ucha Mungu si katika mwezi huo pekee. Majaliwa alisema: “Magufuli ameniagiza kwa Waislamu ni kielelezo cha taasisi za dini zinazozingatia maadili mema, hivyo wachache wasijipenyeze na kuharibu taswira yao.” “Ninawahakikishia kuwa serikali iko tayari kushirikiana na taasisi yoyote ya dini ambayo itakuwa tayari kuzingatia matakwa ya katiba, sheria na taratibu za nchi,’’ alisema Majaliwa. Awali, Sheikh Mkuu, Mufti Abubakar Zubeir alitoa wito kwa masheikh wa mikoa na wilaya zote nchini wahakikishe kila wanapofanya mikutano yao mada ya amani na kudumisha uzalendo zisikosekane kwa kuwa ni maelekezo muhimu. ”Kama mtu hana uzalendo hata dini inapungua, tujenge uzalendo kwa ajili ya kuienzi nchi na kuifanya iendelee kuwa kisiwa cha utulivu…Tuendelee kujenga umoja na mshikamano tusiliache suala hili kwa sababu ndilo liloijenga jamii yetu,’’ alisema,” Mufti Zubeir. Na Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi kutoka Zanzibar, Haji Mtumwa anaripoti kuhusu Eid el Fitr kwa kichwa cha habari, Dk Shein awapa wananchi matumaini ya maisha bora. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amesema nia ya serikali ni kuona kila mwananchi anakuwa na uwezo wa kifedha wa kununua anachohitaji. Dk Shein alisema hayo Ijumaa, Juni 15, 2018 alipokuwa akihutubia wananchi kupitia Baraza la Eid el Fitr lililofanyika katika Ukumbi wa Idriss Abdulwakili, Kikwajuni Mjini Unguja. Akizungumza katika baraza hilo, alisema ni vyema wananchi wakaondoa shaka kwani serikali ipo katika harakati za kuhakikisha malengo hayo yaliyokusudiwa yanafikiwa. “Licha ya serikali kuwa na mpango huo, hakuna budi kupongezwa kwa umoja uliopo kati ya wafanyabiashara na wananchi hasa katika kipindi cha Ramadhani ambacho matumizi yalikuwa makubwa kwa kila mmoja wetu,” alisema Dk Shein. Aliwatahadharisha vijana kuacha tabia ya kuchagua kazi hasa kwa kutaka ajira serikalini au za vikosi vya ulinzi, akisema nia ya serikali ni kuona vijana wanakuwa na ajira hata za kujitegemea ikiwamo ufundi. Alisema serikali imeanzisha vyuo maalumu vya ufundi ili kuwapa vijana elimu ya ujasiriamali huku akisisitiza kuwa mfuko maalumu kwa ajili ya mikopo pia upo na kuwataka vijana kuutumia ipasavyo. Dk Shein alisema kwamba kwa mwaka 2018/19 serikali imetenga zaidi ya Sh1.1 bilioni kwa ajili ya kuanzisha programu maalumu ya kuwainua vijana kiuchumi. Awali, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu Zanzibar, Abdallah Talib aliwataka wananchi kuenzi na kuyaendeleza mafunzo yote yaliyopatikana kwenye mfungo wa Ramadhani. The post Waislamu watakiwa kuepuka maneno dhidi ya Rais Magufuli appeared first on Mzalendo.net.

  • mzalendo.net
  • 6 days ago

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:- 1. Bibi Hamida Ahmed Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara ya Zanzibar katika Wizara ya Biashara na Viwanda. 2. Bwana Omar Ramadhan Mapuri ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia, Zanzibar. 3. Bibi Mwanamkaa Abdulrahaman Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar. 4. Dr. Abdul-Nasser Hamed Hikmany ameteuliwa kuwa Mrajis wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira. 5. Bwana Salum Kitwana Sururu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho na Mambo ya Kale katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale. Uteuzi huo umeanza leo tarehe 14 Juni, 2018. Zanzinews The post DK. Ali Mohamed Shein Amefanya Uteuzi wa Taasisi Mbalimbali.. appeared first on Mzalendo.net.

  • mzalendo.net
  • 6 days ago

June 14, 2018 – by Manager Umeandikwa na Haji Nassor, PEMBA SI haba wazanzibar wenzetu hasa wanawake, wanatambua thamani, heshima na ukubwa wa mwezi mtikufu wa Ramadhani, kwa kule kuuyasitiri maungo yao. Kwa ndani ya mfungo huu wa Ramadhani, mwenye juba, lemba kubwa, kanzu pana, au vazi la kuziba uso umaarufu ninja, limekuwa livaliwa ili kuustiri mwili. Kwangu mimi nasema hii ni faraja, na pengine kwa hawa wanaofanya hivyo, ndio wameshaelimika na kutokana kwenye ujinga, kwa huku kuyaficha maungo yao. Suali ambalo limenileta mbele leo hii, ni kuwauliza hawa wanaostiri miili yao kwa kuvaa mitandio, majuba, vilemba vya heshima yalioambana na madira mapana, kwa lengo ya kuficha viongo wataendelea hata baada ya mwezi huu kumalizika? Au wanaofanya hivi, aya zao za kujistiri pamoja na hadithi huwepo ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani pekee, na ukimalizika na hayo maelekezo na makatazo yao, ndio nayo yamefutika. Maana kwa ndani ya mwezi huu mtukufu wa ramadhani, kila mwanamke, imekuwa ni vigumu kuiona ovyo pengine sura yake na hata yale maungo tuliozoea kuyapicga chabo, mwezi wa kula na mchana, sasa je hali hii itaendelea hata baada ya kumalizika Ramadhani. Mbona kwa sasa kivazi cha baadhi ya wanawake hawa hasa wanaojua nini maana ya Ramadhani, kimekua kikivutia na pangine hata sasa kuwatofautisha kati yale wasiokuwa waumini wa dini ya kiislamu na wengine. Ukipanda nao gari wanawake hawa kwa sasa, utajiuliza kama kuna Ijtimai pahala, au wanakwenda kufanya intaviuu ofisi ya Mufti, kumbe laa hasaha, ni kuupokea na kuusikindikiza mwezi ulioshuhwa Qur-an. Inawezekana, vile vijilemba na vijitandio vya kuwarusha moyo wanaume, ambavyo huvaliwa kwa mwezi wa kula na mchana aidha vimeshatiwa moto au wameshapewa watoto wadogo, na pengine sasa wanawake hawa wa kizanzibar wameshamua kuvaa mavazi yanayokwenda na majina yao. Kwa mfano katika kipindi cha kula mchana, vazi alilokuwa akivaa mtu mwenye jina kama la Jackline, Doyosis halikuwa na tofauti na analovaa mtu mwenye jina la Kul-thumu au Aishaa ambapo haya ni majina ya kiislamu kiitikadi. Kwangu mimi nasema, inawezekana sasa kuwa wanazuoni wetu na masheikh, wameshafanikiwa alau kwa upande wa wanawake, kwamba wamesharejea kwenye mavazi yao ya asili yaliokuwa yakificha maungo. Maana, wapo wanaosema hata ukitaka kuacha pombe, sigara na wizi basi mwezi huu mtukufu wa ramadhani ni mwafaka kufanya hivyo, na ndio pengine sasa vazi la wanawake wanalovaa mwezi huu, ndio moja kwa moja hadi maisha yao. Kwa hali hii, hata wale wanaume wenye kuvaa surauali chini ya makalio, ummarufu mlengezo, bila shaka mjifunze sasa kutoka kwa wanawake, jinsi walivyojistiri ndani ya mawezi huu. Na ikiwezekana baada ya mwezi huu kumalizika, kusiweko tena surauali mlegezo, wala kwa watu wazima wanawake kuvaa vilemba na mitandio ya watoto wao, ambayo honesha mashina ya maziwa wakitembea barabarani. Kama hivyo ndivyo, sote tukumbe kuwa, hata baada ya kumalizika kwa mwezi huu mtukufu, bado aya, hadithi na Muumba ndio yule yule, acheni kuvaa vitandio vinayoonesha maumbile yenu. Lakini hata wakuu wa kaya, bado mnawajibu wa kuhakikisha, suala la vazi la stara kwa wanawake na wanaume, linakuwa endelevu hata baada ya kuhitimishwa kwa kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani. Viongozi wetu wa dini, lazima muendelee na jukumu lenu la kuwaelezea waumini wenu, hasara za wasiofunika maungo yao, maana kwa kweli ni hatari jinsi maungo yanavyopigwa jua kama vile mwenyewe amerukwa na akili. Kama hivyo ndivyo lazima kila mmoja, aseme na akili yake akijua kuwa, kama mwezi wa Ramadhani unavyoondoka, hata mimi, wewe, yule na wao wataondoka, je tunajipangaje. Kila kitu kinawezekana iwapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake, kwa kufuata maelekezo na makatazo wa Muumba na huku akijua kuwa, iko siku ya malipo. Pembatoday The post Wanaojistiri kwa Ramadhan, wataendelea hata ikimalizika? appeared first on Mzalendo.net.